Kurasa

Jumatatu, 21 Oktoba 2013

SONY MUSIC KUMTOA RASMI ROSE MUHANDO MWISHONI MWA MWAKA HUU

Source: Uncle Jimmy

Kushoto ni Seven Mosha,Rose Muhando na muwakilishi wa Sony Africa...Picha hii walipiga february mwaka jana kwenye hafla ya kusaini mkataba huo.

Mkurugenzi wa vipaji na Biashara Seven Mosha amesema kampuni kubwa ya muziki dunia (SONY MUSIC AFRICA) iliyo ingia mkataba na muimbaji Rose muhando mwishoni mwa mwaka huu kazi mpya za Rose Muhando zitaanza kutoka.Amesema kipindi chote mwana muziki Rose Muhando alikua akirekodi nyimbo mpya kwenye studio za Sony Music Afrika zilizopo nchini Adrika Kusini.

Seven amesema nyimbo za Rose akiwa nchini ya label hiyo zitaendelea kuwa zile zile zilizo zoeleka kwa watu wengine lakini kilichobadilika ni ubora wa utayarishaji."Producer ambao alifanya nao kazi ndio hao hao,ni studio tu zilizotumika South Africa.Kwahiyo timu yake nzima ya production tulienda nayo South Africa"amesema.
Akieleza tofauti aliyonayo Rose kwa sasa,Seven amesema kipaji chake kiko pale pale na wamekiboresha zaidi kuwa na hadhi ya kimataifa na uwezo wa kuitumia sauti yake vizuri zaidi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni